This is the current advice on coronavirus in Scotland

Ili kujilinda sisi wenyewe na kuilinda NHS dhidi ya virusi vya Corona, ushauri wetu hapa Scotland ni ule ule.

Hii ni kwa sababu ushahidi unatuonyesha bado ni mapema sana kufanya mabadiliko makubwa.

Kwa hiyo mabadiliko pekee yanayopendekezwa ndani ya Scotland ni kwamba unaweza kutoka nje kufanya mazoezi, karibu na nyumba yako, zaidi ya mara moja kwa siku, kama tu utabaki katika eneo lako.

Kwa kuendelea kubakia ndani unailinda NHS ndani ya Scotland, na kuokoa maisha.

Unatakiwa kuendelea kukaa umbali wa mita mbili na mtu mwingine unapokuwa nje ya nyumba yako na uoshe mikono yako unaporudi nyumbani.

What's your reaction?
0cool0bad1lol0sad